Darasa la kupigilia pamba kijanja!

Habari wakuu,
Nimeona na mimi nitoe darasa kidogo kuhusu
mavazi sababu na mimi ni kipaumbele changu
katika maisha.
1.Epuka kuvaa marangirangi
Wakati unamatch mavazi jitahidi kupunguza
idadi ya rangi,rangi 3 tu zinatosha kukutoa
bomba.
2. Vaa kulingana na mazingira/sehemu
Mtu mjanja anajua kubadilika kulingana na
mazingira,sio kuvaa jezi la Man utd lenye jina la
Wazza kwenye sherehe
3. Masharti ya kuchomekea;
* Marufuku kuvaa oversize/undersize
* Usivae mlegezo
* Hakikisha singlet haionekani
* Usivae mkanda mrefu
* Usivae makubanzi/sandals
* Hakikisha umemach rangi
4. Kama umevaa pensi /kaptula...
* Hakikisha unavaa soksi fupi zisizoonekana
* Piga raba au makubanzi/sandals bila soksi
* Haipendezi kuchemekea
* Hakikisha miguu ni soft
5. Usivae shati jeupe kama la mwanafunzi
Shati nyeupe ni nzuri kama unaijulia wakati
unanunua hakikisha ina urembo wa aina yoyote
ile au ni ya kimtindo sio kuvaa shati la shule.
6. Hakikisha una suruali nyeusi
Mwanaume yoyote yule wa kijanja anajua
umuhimu wa suruali nyeusi sababu inamatch
mashati ya rangi nyingi.
7. Saa
*Kama umevaa jeans/kadet unaruhusiwa kuvaa
saa ya aina yoyote
*km umevaa suti/suruali ya kitambaa epuka
kuvaa saa ya mkanda wa plastic.
8. Miwani
Duh hapa pagumu kidogo lakini cha msingi
zingatia muundo wa kichwa chako pamoja na
aina ya macho uliyonayo na aina ya pamba
ulizovaa pia.Sio umepiga jeans kali,kichwa kama
madenge na macho kama bundi kisha unapiga
miwani ndogo ya njano,ni kituko
9/.Vaa kofia za kijanja
Kofia pia huongeza mvuto,chagua kofia kulingana
na aina ya kichwa na mavazi uliyovaa,haipendezi
kuvaa suti na kapelo.Kanzu sharti ivaliwe na
barakashia ndo utaeleweka la sivyo ni sawa na
kuvaa dera tu
10/Mkanda
*Usivae mkanda mrefu km vile umefunga nyoka
kiunoni
*Mikanda ya vitambaa au madoidoi inafaa
kuvaliwa na jeans/kadeti/kaptula
*Jitahidi mkumatch rangi ya mkanda na viatu
kama umevaa nguo za kuchomekea
*Zingatia upana wamkanda na rux za nguo yako
11/ Tupia cheni za ukweli
Mikufu ya kiume pia huongeza mvuto
* Kama umevaa nguo za kuchomekea au suti
itapendeza ukivaa cheni nsogo ambayo haitokezi
nje ya shati
*Kama umepiga pamba za Joshua mfano T.shirt
na jeans hapa tupia cheni kubwa lakini hata
cheni ndogo zinakubali
12/Uvaaji wa Tie
*Vaa kulingana na urefu wako
*Km wewe mwembamba inapendeza kuvaa tie
nyembamba
*Jitahidi kumatch tie na rangi ya shirt/suruali
*Hakikisha tie yako imefungwa vizuri shingoni
13/T.shirt na Jeans
Wanaume wajanja wa mjini hupenda kupiga t
shirt na jeans na chini kutupia raba Kali.....Vazi
hili lina mvuto wa aina yake hasa limivaliwa
kitaani na sehemu za mitoko km vile kwenye
Club za starehe
14/Vaa viatu kijanja
Hapa pia Kuna changamoto
*Usivaa suruali ya kitambaa na Raba
*Usivae suruali ya kuchomekea na makubanzi
*Ukipiga jeans unaweza kumatch t.shirt/shirt na
rangi ya viatu
*Ukivaa suti yakupasa upige kiatu kikali
....ulikosea itakuwa sawa na Toyota Mark X
yenye matairi ya Fuso !!!
***Usipojua kuvaa utadharaurika***

Comments

Popular Posts