Waziri Ndalichako katolea ufafanuzi kufukuzwa kwa wanafunzi wa UDOM
Jumatatu hii Naibu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson amelazimika kusitisha shughuli za bunge hilo kabla ya muda baada ya wabunge kugoma wakitaka wajadili suala la wanafunzi walioondolewa kwenye chuo kikuu cha Dodoma, UDOM.Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ilitangaza kuwafuza jumla ya wanafunzi 7802 kutoka Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kufuatia mgomo wa Walimu unaoendelea hivi sasa. Waziri Joyce Ndalichako amesimama Bungeni leo kuongelea suala hilo. Hatahivyo bado suala hilo halijafikia mwisho baada ya wabunge kutoka nje ya bunge
Posted via mwanzaniani.blogsport.com

Comments
Post a Comment